×

Vita Ukraine Kumalizwa

MAZUNGUMZO pekee ndiyo yanatazamiwa na wengi kuwa ni njia bora ya kumaliza vita vilivyozuka siku tano zilizopita kati ya Urusi na Ukraine.

 

Tayari wajumbe kutoka nchi hizo mbili wameanza mazungumzo yenye lengo la kumaliza vita hivyo inayotia hofu ulimwengu mzima.

Ofisi ya rais wa Ukraine inasema inataka kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuondolewa kwa vikosi vya Urusi.

Moscow kwa upande wake inataka kufikia makubaliano ambayo yalikuwa kwa maslahi ya pande zote mbili, kulingana na mpatanishi wa Urusi, Vladimir Medinsky.

 

Kabla ya mkutano huo kuanza, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky aliwataka wanajeshi wa Urusi kuweka chini silaha zao na kutoa wito kwa EU kuipatia Ukraine uanachama wa umoja huo mara moja.

Stori: Richard Manyota

Leave a Comment