×

Pablo Ataja Mechi Mbili za Kutinga Robo Fainali CAF

MARA baada y kufungwa dhidi ya RS Berkane ya nchini Morocco, Kocha Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amesema ili wafuzu robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, lazima washinde michezo miwili ya nyumbani.

 

Simba wanautumia Uwanja wa Mkapa uliopo Dar kama uwanja wao wa nyumbani katika michuano hiyo wakiwa hatua ya makundi ambapo mechi ya kwanza kucheza hapo waliifunga ASEC Mimosas mabao 3-1.

 

Ikiwa tayari imecheza mechi tatu, moja nyumbani na mbili ugenini, imebakiwa na tatu zikiwa mbili nyumbani dhidi ya US Gendarmarie na RS Berkane, huku moja ugenini itakuwa dhidi ya ASEC Mimosas.


Pablo amesema katika mechi hizo tatu, anahitaji kushinda mbili za nyumbani na sare ugenini kujihakikishia nafasi ya kwenda robo fainali.

 

“Tumekubali kupoteza ugenini, lakini katika michezo mitatu tumekuwa timu pekee ambayo imepata pointi ugenini, tuna michezo miwili nyumbani.

 

“Malengo yetu ni kushinda michezo yote mwili ya nyumbani na kutafuta pointi moja ugenini dhidi ya ASEC Mimosas ambao tuliwafunga nyumbani,” alisema Pablo.

ITAKULIZA! UJUMBE WA MWANAJESHI WA URUSI KWA MAMA YAKE KABLA YA KUUAWA, BALOZI WA UKRAINE AUSOMA…

Leave a Comment