
Mchungaji Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ na wenzake 92 leo Machi 3, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza na kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayokabili.
Msafara wa magari matatu aina ya difenda zilizolindwa na askari waliojihami kwa silaha umewasili katika mahakama hiyo saa 9:00 mchana kisha watuhumiwa hao kuamuriwa kuingia ndani ya mahakama hiyo.
Akishuka katika gari ya polisi iliyokuwa imembeba, Zumaridi amesikika akisema “Mimi ndiyo Mfalme Zumaridi” huku akionyesha ishara ya kuomba.
Shitaka lingine linalomkabili Zumaridi ni Kesi namba 11 ya mwaka 2022, ambapo Zumaridi anatuhumiwa kwa kosa la usafirishaji wa Binadamu. Zumaridi pia anatuhumiwa kwa kosa la tatu akiwemo yeye na wenzake 84 ambapo ni kesi namba 12 ya mwaka 2022, kwa tuhuma za kufanya kusanyiko lisilo halali, pamoja na tuhuma za kushambulia Mwili.
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx