×

Kanye Na Kim Ni Rasmi Sasa

ILIKUWA miaka ikafuata miezi kisha siku na sasa ni rasmi kwamba baada ya muda mrefu wa kuvurugana katika ndoa yake na msanii Kanye West, mwanamitindo Kim Kardashian sasa ni rasmi kuwa amehalalishwa kulifutilia mbali jina la Kanye West kwenye dokyumenti zake.

Hii ni baada ya kushinda kesi aliyoiwasilisha mahakamani kutaka kutangazwa rasmi kuwa single na hayupo tena na Kanye West.
Kesi hiyo ambayo aliiwasilisha mahakamani mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuachana, ilipata pingamizi kubwa kutoka kwa Kanye West ambaye alikataa kabisa Kardashian kutangazwa kuwa single kwa kile alichokisema bado anampenda na hata kumtaka arudi ili wazidi kulea watoto wao pamoja, jambo ambalo Kardashian alikataa kabisa na kuendelea mbele na kesi ya talaka na kutanga iwekwe rasmi kwamba hayupo katika mahusiano na West tena.

 

Wawili hao wamekuwa katika mahusiano ya ndoa tangu mwaka wa 2012 na kubarikiwa watoto wanne lakini mwaka jana Kardashian alimtuhumu Kanye West kwa kile alichosema ni unyanyasaji.

Leave a Comment