
Hilali Shaweji Makarani ‘Shehe Kipozeo’ amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali wito wa kuzungumza na viongozi wa dini.
Amesema Rais Samia ni msikivu, si mbaguzi na mwenye kuwajali watu ambapo aligusia pia suala la busara kuhusu kesi iliyokuwa ikimkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye leo March 04, 2022 amechiwa huru baada ya DPP kufikisha hati ya kutoendelea na kesi mahakamani.