×

Uwoya: Sijui Natumia Pesa Kiasi Gani

IRENE Uwoya; ni mwanamama mwenye pesa zake kunako Bongo Movies; yeye anasema kuwa, hawezi kusema ni kiasi gani cha pesa anachotumia kula bata.

 

Majibu hayo yamezuka baada ya kuulizwa anawezaje kuhudumia watu wengi anaotembea nao kila anakokwenda huku wakiwa wanakaa kwenye hoteli za gharama kubwa.

 

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya anasema kuwa, inategemea, lakini cha msingi ni kuinjoi maisha.

 

“Mara nyingi huwa siwezi kujua ni kiasi gani cha pesa kwa sababu huwa sipendi kuongelea sana hilo suala kwamba eti natumia kiasi gani, inategemea na bata lenyewe linafanyikia wapi,” anasema Uwoya ambaye anakuambia pesa haitafutwi, bali inategwa.

Leave a Comment