×

Mbowe Afunguka Alichozungumza na Rais Samia – Video

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe, leo Machi 08, amehutubia kwa mara ya kwanza kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyoandaliwa na Baraza la wanawake la Chadema (Bawacha).

 

Mbowe ametumia siku ya wanawake kupitia Kongamano la Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) kuzungumza na Watanzania kuhusu mambo mbalimbali ikiwamo kesi ya ugaidi iliyokuwa inamkabili.

 

Amesema kesi ilipofutwa alipokea ujumbe wa Rais Samia kutaka waonane, naye hakusita kwa sababu chama chake kilikuwa kinasubiri nafasi hiyo.

 

“Kwa sababu mbalimbali niliridhia, kwanza binafsi na chama chetu tumetafuta nafasi hiyo bila mafanikio. Rais wa mwisho kukaa naye alikuwa Jakaya Kikwete,” amesema Mbowe na kuongeza:

 

“Kwa hiyo tumetafuta fursa ya kuonana viongozi kwa sababu tunajua wana-Chadema wamebeba nini vifuani mwao na tunaamini Rais ndiye mwenye funguo ya vikwazo vingi zinavyosababisha simanzi kwenye Taifa.

 

Kiongozi huyo wa Chadema amesema hakuruhusu uchungu vimpe kiburi kwa kushindwa kuonana na Rais Samia japo na yeye alijiuliza aanze na mguu upi.

 

“Wakati wote nilipokuwa gerezani niliomba kibali na nilikiona kibali hiki nilipopata mwaliko hivyo, zangu nilikwenda Ikulu. Nimshukuru Rais Samia kwa sababu alinipa pole, na namshukuru kwa namna mazungumzo yetu yalivyokwenda,” amesema.

 

Ameeleza kuwa Samia amekuwa Rais wa kwanza wa Taifa kusimama hadharani kuzungumza na vyombo vya habari kwamba, wafanye nini kila mmoja kwa chama chake kuondoa maumivu yaliyo katika taifa hilo.

Leave a Comment