×

Mzee wa Miaka 69 Hatiani kwa Mauaji

Mtuhumiwa wa mauaji, Marima Mazengo (69) akitoka katika chumba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha nje.

 

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, imemhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja, Marima Mazengo (69) baada ya kukutwa na hatia ya mauaji ya bila kukusudia ambapo ameamriwa kutotoka nje ya mkoa wake pasikokuwa na kibali maalum na kutotenda kosa lolote kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja.

 

Awali, mtuhumiwa huyo akisomewa maelezo ya kosa na mwendesha mashtaka wa serikali, imedaiwa kuwa mnamo Desemba 14, 2017 akiwa katika Msitu wa Chamangwe uliopo eneo la Makondeka Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, alimuua marehemu Michael Shadrack kwa kumkatakata mapanga .

 

Mara baada ya kusomewa shtaka hilo mbele ya Jaji Edwin Kakolaki aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, mtuhimiwa alikiri kutenda kosa hilo.

 

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Kakolaki amesema kuwa kwa kuzingatia mauaji hayo ni kwamba amesikiliza pande zote ambapo marehemu mwenyewe alichangia kutokea mauaji hayo kwani kitendo cha yeye kutaka kumnyang’anya mbwa wake ndicho kilichosababisha mtuhumiwa kujawa na hasira na kumkata mapanga kwa kujihami.

 

Akaeleza kuwa kwa kuzingatia hilo, japokuwa marehemu alikuwa na haki ya kuishi lakini sasa na kwa kuangalia mshtakiwa amekaa gerezani kwa takribani miaka minne na umri wake umeenda, hivyo akaamua kumhukumu kifungo cha nje cha mwaka mmoja.

 

Leave a Comment