
Kundi la wanafunzi 11 waliokuwa wamekwama Sumy nchini Ukraine wameokolewa na kufikishwa salama katika Ubalozi wa Tanzania jijini Moscow, Urusi.
Wanafunzi hao wanaonekana wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Frederick Kibuta na maafisa ubalozi baada ya kuwasili salama Moscow.
taarifa zaidi zinaeleza kuwa kundi la Watanzania wengine zaidi ya 50 ambao walikua wamekwama kwenye Mji wa Sumy nchini Ukraine kwa zaidi ya siku 10 kutokana na vita, wameanza kuondoka kwenye mji huo kuelekea kwenye mji wa jirani wa Poltava ambako wanatarajia kupanda treni mpaka nchini Poland.
Kiongozi wa kundi hilo, Dkt. Lahsen Mohammed Kheir amesema kwamba chuo chao kimewapa mabasi ya kuwasafirisha bure hadi Poltava ambako zinapatikana treni za uokoaji zinazopeleka watu kwenye mipaka ya Ukraine na Hungary na Poland.