×

Diamond: Kama Mrabaha tu Huwezi Kunipa, Tuzo Utanipa ?

Msanii kiongozi katika tasnia ya Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema iwapo hapatiwi mirabaha na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) itakuwaje apewe Tuzo za Tanzania Music Awards zinazoandaliwa na Serikali.

Diamond amesema hayo jana Jumatatu, Machi 14, 2022 wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika na Kituo cha Radio cha wasafi FM alipofika kwa ajili ya kutambulisha EP yake mpa inayokwenda kwa jina la FOA (First of All) ambayo aliiachia rasmi usiku wa kuamkia machi 11, 2022.

“Kimsingi Rais wetu Mh. Samia Suluhu ana nia njema sana ya kuwasaidia wasanii. Lakini kama kuna watu wamepewa nafasi huku chini kushughulikia mirabaha inabidi waangaliwe wasije kuitia doa serikali na nia yao njema. Kwa mfano kama mrabaha tu huwezi kunipa je, tuzo utanipa ?” amesema Diamond.

Ikumbukwe kuwa Diamond ni miongoni mwa wasanii wakubwa nchini ambao hawajapewa mirabaha na COSOTA licha ya kazi kubwa anayoifanya na umaarufu wake huku ikielezwa chanzo cha kukosa mirahaba ni kwa kuwa nyimbo zake hazichezwi na vyombo vingi vya habari nchini.

KUSIKILIZA #FOA EP INGIA HAPA ==> #FOAtheEP

Leave a Comment