
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amesema nchi ilishapiga hatua kwenye suala la Katiba Mpya kwani ilishakubaliana Mwaka 2014 na kuunda Tume.
Amesema hayo baada ya kuulizwa mawazo yake kuhusu Katiba Mpya inayoonekana kudaiwa na wapinzani. Ameeleza, swali la kujiuliza ni lini mchakato wa Katiba Mpya ulioainishwa utarejewa na kumalizwa kwani Nchi imeshatumia Rasilimali nyingi.
“Tulishakubaliana kama nchi kuwa tunataka Katiba Mpya tangu mwaka 2014 ndiyo maana tukaanzisha mchakato wa Katiba na kupata Katiba inayopendekezwa, tunachopaswa kuzungumza kwa sasa ni nili tunaendelea na mchakato na siyo kurudisha mambo nyuma,” amesmea Prof. Kitila.