
Katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa mwanamuziki Harmonize ametangaza kuja na tamasha lake la #OneLoveConcert lenye dhumuni ya kuchangia na kufurahia na watu wenye mahitaji maalumu mnamo Machi 20,2022, Mlimani City, Dar es Salaam.
Kupitia taarifa yake aliyo-share katika ukurasa wake wa Instagram, Harmonize ameleeza kuchangia kiasi cha Tsh million 2 huku akitaka kuungana na wadau na mashabiki mbalimbali kuchangia chakula, nguo, fenicha, vyombo pamoja na fedha kuanzai kiasi cha Tsh shiling 1,000/= na kuendelea.
Ikumbukwe kuwa, enzi za uhai wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Hayati Reaginard Mengi alikuwa na taasisi iliyokuwa ikishughulikia matatizo ya ya watoto wenye uhitaji maalum, hivyo Harmonize anamuenzi mzee mengi kwa kujitoa kuwasaidia wenye uhitaji.