×

Manara Awalipua Wachambuzi, Atangaza Matukio Makubwa – Video

 

OFISA habari na msemaji wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli na Haji Manara, wamezungumza na wanahabari leo Machi 16, 2022 kuhusiana na suala la mchezaji wao wa Yanga Princess, Aisha Masaka kuuzwa nje ya nchi na kuelekea mchezo wa ligi kuu utakaochezwa Machi 19, 2022.

 

Aidha wametangaza kuwa kesho Machi 17, 2022 watatembelea hospitali ya Ocean Road na kutoa msaada ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Hayati Magufuli, afariki dunia.

 

“Kutakuwa na Mechi ya Utangulizi kati ya Wafanyakazi wa Yanga na Wasanii ikiambatana na Burudani Kubwa kutoka kwa Wasanii wakubwa pia Uongozi wa Young Africans SC umemualika Rasmi Mh. Rais Mama yetu Samia Suluhu Hassan kuja kushuhudia mchezo wetu dhidi ya KMC katika kilele cha Mwaka Mmoja wa Urais wake”

“Jambo lingine mahususi ni Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais wetu Samia Hassan Suluhu ambayo kilele chake ni siku ya Jumamosi tarehe 19/03/22, pia kuelekea maadhimisho ya Mwaka 1 wa Rais wetu Wapenzi, Wanachama na Mashabiki wa Young Africans SC tukutane Benki ya Damu iliyopo Hospital ya Muhimbili tukachangie Damu na Wanayanga 200 wa kwanza watapata zawadi ya Jezi”
“Kuelekea kumbukumbu ya Mwaka Mmoja wa kifo cha Rais Magufuli tunaungana na Watanzania wenzetu kwa kutembelea Hospital ya Ocean Road tukishirikiana na GSM Foundation kama sehemu ya kumuenzi”
 
“Kwenye mchezo wa hisani wa Ali Kimara Rare Diseases Foundation tunapenda kuwashukuru sana Serikali kupitia Wizara husika, TFF kama wenye mpira wao na vyombo vyote vya habari pamoja na Wanachi waliojitokeza na waliotizama kupitia TV”  amesema Msemaji wa Young Africans SC, Haji Manara

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment