
ESMA Khan almaarufu Esma Platnumz; ni dada wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz ambaye baada ya kuwepo kwa tetesi kwamba anaendesha maisha kwa pesa za kaka yake huyo, ameibuka na kukana madai hayo.
Esma anasema kuwa, kamwe hajawahi kukubali kujibweteka eti kwa kuwa kaka yake ni tajiri mkubwa.
Anasema kuwa, huwa anafanya kazi kwa bidii kujitafutia pesa zake mwenyewe.
“Ulimwengu wa sasa hivi huwezi kumtegemea kaka yako, baba yako au ndugu yeyote. Unatakiwa kama mwanamke usimame mwenyewe. Mimi nina watoto na wananiangalia. Mtoto wangu atachukuaje mfano kutoka kwangu?
Atasema alale jinsi mama’ke alivyolala? Hata watoto wangu nikikaa nao huwa nawapa mifano. Huwa nawaambia wasikae wajibweteke kwa kuwa mjomba wao ana pesa, hapana.
“Mimi najitafutia pesa kwa ajili ya watoto wangu naye Naseeb (Diamond) anajitafutia pesa kwa ajili ya familia yake. Ni vitu viwili tofdauti,” anasema Esma ambaye ni mama wa Watoto wawili.