Rais Samia Aongoza Watanzania Kuadhimisha Mwaka Mmoja wa Hayati Magufuli -(Picha +Video)
Global Publishers March 17, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wananchi wa Chato pamoja na Wageni kutoka Sehemu mbalimbali nchini katika Kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika uwanja wa Michezo wa Magufuli leo tarehe 17 Machi, 2022.
LEO Alhamisi, Machi 17, 2022 ni siku ya kumbukizi ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya 5 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Kumbukizi hiyo inafanyika kitaifa katika Viwanja vya Magufuli, Chato mkoani Geita ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anawaongoza Watanzania kumkumbuka na kumuenzi kiongozi huyo shujaa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika uwanja wa Michezo wa Magufuli leo tarehe 17 Machi, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha kumbukumbu kabla ya kuweka Shada la Maua katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Kumbukizi ya mwaka mmoja tangu kufariki dunia kwa Hayati Dkt. Magufuli leo tarehe 17 Machi, 2022.
Matukio katika picha kutoka Chato mkoani Geita kwenye Uwanja wa Magufuli ambapo kunafanyika Ibada ya Kumbukizi ya Kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli leo Machi 17, 2022.