×

Urusi Yadai Kuwauwa Wanajeshi 100 wa Ukraine Schytomyr

Shambulio la Urusi katika kituo cha mafunzo cha karibu na mji wa kati wa Ukraine wa Schytomyr linadaiwa kuwaua wanajeshi 100 wa Ukraine na wengine wa kigeni. Hayo ni kwa mujibu wa habari za Urusi ambazo hazijathibitishwa.

 

Taarifa hizo zinatolewa katika kipindi ambacho kwa siku ya pili jeshi la Urusi linaripotiwa kutumia silaha nzito za makombora ya masafa marefu ya Kinshal tangu livamie Ukraine.

 

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, Igor Konashenkov amesema shambulizi hilo lilifanyika katika kituo cha kijeshi cha Mkoa wa Mykolaiv.

 

Serikali ya Urusi imesema kituo hicho kilikuwa muhimu kwa ajili ya ujazaji wa mafuta kwa mizinga ya Ukraine.

 

Na kadhalika wamelipua karakana ya ukarabati wa mizinga hiyo. Hata hivyo, bado haijawa wazi ni silaha gani zimetumika katika shambulizi hilo la Schytomyr.

UPDATES: AJALI NYINGINE ILIYOUA WATU 2 MORO, KAMANDA MUTAFUNGWA AZUNGUMZA..

Leave a Comment