×

Mondi: Video 10 kwa mpigo

NASIBU Abdul almaarufu Diamond Platnumz au Simba, ametangaza rasmi maangamizi ya kuonesha wasanii wa Afrika Mashariki wamepania kufanya vizuri mno mwaka huu.

 

Diamond au Mondi anasema kuwa, tayari amefanya video za nyimbo zote 10 zinazopatikana kwenye albam yake fupi (EP) ya First Of All (FOA).

 

“Natamani niwambie kitu kimoja, EP ina video zote 10, video zake ni kali sana, video zake zimekaa ‘hatucheki na kima’, yote ni kuonesha kwamba wana Afrika Mashariki tupo vizuri,” amesema Diamond ambaye EP yake hiyo inaendelea kuweka rekodi za kila aina kwenye platforms (majukwaa) mbalimbali ya muziki duniani.

Stori; Mwandishi Wetu, Dar

Leave a Comment