×

Bondia Ukraine Aondoka Jeshini Kumuwinda Joshua

BINGWA wa uzito wa juu Oleksandr Usyk ambaye anashikilia mikanda ya WBA, IBF, WBO na IBO amethibitisha kuondoka jeshini na kuanza kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Muingereza Anthony Joshua.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 35 ambaye ni raia wa Ukraine, alikuwa jeshini akisaidia kuilinda nchi hiyo baada uvamizi wa Urusi.

“Niliamua kuanza kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Anthony Joshua,” Usyk aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram

Usyk alijiunga na jeshi la Ukraine mnamo Machi kufuatia uvamizi wa Urusi Usyk, anatazamiwa kumenyana na Joshua mwezi Julai .

Leave a Comment