×

IGP Sirro Afanya Mabadiliko ya Makamanda wa Polisi – Video

Kamanda wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro, amefanya uhamisho na mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi huku aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Wankyo Nyigesa akihamishiwa makao makuu.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime imeeleza kuwa Kamanda Nyigesa amehamishiwa makao makuu ili kupisha uchunguzi wa tukio la Machi 26, 2022 alilolifanya katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ambapo inadaiwa kuwa alitoa maneno ambayo yanaonyesha ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya jeshi la polisi.

Siku chache zilizopita, video inayomuonesha Kamanda Wankyo Nyigesa ilianza kusambaa kwa kasi ambapo anasikika akieleza kwamba anatamani kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).

Leave a Comment