Benki Kuu ya Ethiopia, Safaricom Ethiopia Wajifunza Namna Huduma za M-Pesa Zinavyofanyakazi
Global Publishers March 29, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
MKURUGENZI wa Vodacom M-Pesa, Epimack Mbeteni (kushoto) akiwaelimisha maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Plc, Sitholizwe Mdlalose akizungumza na maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna huduma za kifedha kwa njia ya mtandao zinavyoleta tija kwa jamii na kuongeza pato la taifa kwa kufuata sheria na mamlaka husika za nchi. Ujumbe huo umekuja jijini Dar es salaam kwa lengo la kujifunza huduma jumuishi za kifedha kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi.
Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Brigita Shirima akiwa kwenye kituo cha mafuta kwa ajili ya kuwaonesha maofisa kutoka benki kuu ya Ethiopia (National Bank of Ethiopia) na kampuni ya simu za mkononi ya Safaricom Ethiopia namna ambavyo wateja wanaweza kulipia kwa kutumia huduma ya “Lipa kwa simu” ikiwa ni sehemu ya kuwaonesha namna huduma ya kulipa kidijitali kupitia M-Pesa inavyofanya kazi.