×

“Awamu ya 5 Ilikuzwa Heshima ya Woga, Kulikuwa na Simba wa Yuda”-Rais Samia

 

Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye hafla ya uapisho wa viongozi wateule Ikulu Chamwino Dodoma leo Aprili 2, 2022

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kuwa awamu ya tano ilisifiwa kwa kuleta heshima ndani ya utumishi wa umma lakini heshima hiyo ilikuzwa kwa misingi ya woga.

 

Rais Samia ameyasema hayo leo Aprili 2, 2022 wakati wa hafla ya uapisho wa viongozi wateule wakiwemo mawaziri watatu waliohamishwa wizara.

 

Tunasifiwa kwamba adjustments (marekebisho) tuliyoyafanya awamu ya tano yameleta heshima ndani ya utumishi wa umma. Heshima iliyokuzwa ni ya woga kwa sababu kulikuwa na Simba wa Yuda, ambaye alikuwa ukigusa sharubu anakurarua, heshima inayotakiwa iwe ya moyoni.

Leave a Comment