×

Foward Motion Yatoa Elimu ya Afya ya Uzazi na Hedhi Salama Kwa Yatima

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Forward Motion, Vivian Sirikwa akizungumza kwenye mafunzo hayo.

 

 

TAASISI ya Forward Motion inayojihusisha na utoaji na uhamasishaji wa elimu ya afya ya uzazi na hedhi salama kwa kushirikiana na madaktari bingwa, leo wameetoa elimu hiyo kwa mabinti wanaolelewa kwenye vituo vya yatima jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Forward Motion, Vivian Sirikwa amesema wameamua kutoa elimu hiyo kwa mabinti hao ili kuwakinga na changamoto mbalimbali za afya ya uzazi na hedhi salama inayoweza kuwakuta kwenye mazingira wanayoishi.

Mabinti yatima wakipewa elimu ya afya ya uzazi na hedhi salama kutoka kwa daktari.

 

 

Akiendelea kuzungumza kwenye mafunzo hayo Mkurugenzi Vivian amesema;

“Katika huu uelimishaji tulianza na utafiti na kuja na kampeni iitwayo Tupa Kitambaa Jali Afya Yako.

“Hii ni kampeni inayohamasisha matumizi ya taulo za kike za kisasa kwa maana utafiti wetu umebaini kuwa asilimia 27 ya wanawake wa kitanzania ndiyo wanaotumia taulo za kike za kisasa na wengine wote wakati wa hedhi wanatumia vitambaa ambavyo si salama kiafya.

Mmoja wa mabinti akiuliza swali kuhusiana na afya ya uzazi na hedhi salama.

 

 

“Unakuta wengine wanatumia vitambaa ambavyo havina usafi unaokidhi viwango na madhara mengineyo.

“Katika kutambua hilo ndiyo maana leo tumeamua kuungana na mabinti hawa ili kuwapa elimu ya afya ya uzazi na hedhi salama ili wao ndiyo wakawe mabalozi wa kutoa elimu hii kwa mabinti wenzao na wanawake wengine kwa ujumla.

Mkurugenzi Mtendaji wa Foward Motion akigawa misaada kwa mabinti hao baada ya mafunzo hayo.

 

 

“Pamoja na elimu hiyo taasisi yetu imetoa msaada wa vyakula kwa watoto hawa kwa ajili ya kujiandaa na mfungo mtukufu wa Mwezi Ramadhani,” alimaliza kusema Mkurugenzi Vivian.

Pichani baadhi ya mabinti hao wakiwa na wageni wa meza kuu.

 

 

Akizungumza kwa niaba ya walezi wa vituo vya yatima hao, Ustaadh Abdallah Abuu kutoka kituo cha Al Hidaya cha Buguruni, Dar ameisifu kwa taasisi ya Forward Motion kwa kuwapa mabinti hao elimu hiyo ambayo imewafanya wajitambue zaidi na kuweza kuwa mabalozi wa kutoa elimu hiyo kwa mabinti na wanawake wengine kwa ujumla.

Mlezi wa Kituo cha Yatima Al Hidaya kilichopo Buguruni Dar, Ustaadh Abuu akitoa shukrani zake kwa taasisi ya Foward Motion kwa kuwapa mabinti hao elimu hiyo pamoja na misaada ya chakula waliyopewa.

 

Pia kwa niaba ya walezi wenzake wa vituo hivyo ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada wa vyakula iliyowapatia.                                                                                                                                                                                                              HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave a Comment