×

Gwiji wa Soka Matt Le Tissier ajiuzulu Ubalozi Kisa Vita ya Ukraine na Urusi

                     Matt Le Tissier Gwiji wa zamani wa Klabu ya Southampton ya nchini Uingereza

GWIJI wa Soka aliyewahi kuwika na klabu ya Southampton na timu ya taifa ya Uingereza Matt Le Tissier amejiuzulu nafasi yake ya ubalozi wa Klabu ya Southampton kutokana na kuhoji ukweli wa taarifa zinazoandikwa na vyombo vya habari kuhusu mauaji ya raia nchini Ukraine.

 

Katika ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter Le Tissier aliandika:

 

“Vyombo vya habari vilidanganya kuhusu zana za maangamizi, vyombo vya habari vikadanganya kuhusu Uviko-19, vyombo vya habari vilidanganya kuhusu Komputa ya Joe Biden, lakini sasa naona vyombo vya habari vimesema ukweli kuhusu mauaji ya Bucha.”

                                                 Matt Le Tissier ajiuzulu Ubalozi wa Klabu ya Southampton

Kauli hiyo ya Le Tissier imetafsiriwa kuwa ni ya kejeli kwa wananchi wa Ukraine na imezua mjadala mkubwa sana mitandaoni kufikia hatua ya gwiji huyo kuifuta na kuitolea ufafanuzi kuwa alieleweka vibaya.

 

Baada ya kujiuzulu Le Tissier ambaye ni raia mzawa wa nchi ya Uingereza amesema mitazamo yake siku zote haibadili na anachokiamini yeye hawezi kubadilishwa na mtu mw

Leave a Comment