
WAZIRI wa Nishati January Makamba amesema kwamba kwa sasa Tanzania hakuna uhaba wa Mafuta licha ya bei kupanda ambayo inachangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta soko la Dunia.
Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam katika Kikao Kati ya Wizara, waagizaji na wasambazaji wa mafuta hapa nchini ili kuangalia namna ya mwenendo wa biashara hiyo.
Waziri Makamba amesema kuwa wamejitahidi sana kusimamia mfumo wa Mafuta ambapo hadi sasa mafuta yaliyopo kwenye Maghala yanatosheleza kwa siku 27 ambayo ni tofauti na yale yanayoshushwa bandarini na yaliyo njiani kuja nchini.
Hata hivyo amesema mafuta yanayotarajia kuingia nchini yanatosheleza kwa siku 33 huku Petroli yakitosheleza kwa siku 37 ambapo kikanunu ni siku 15 na kwa takwimu hizo ni kwamba tayari wamevuka kiwango.
Sambamba na hayo amewatoa hofu watanzania kuwa mafuta yapo na yataendelea kuuzwa kwenye vituo kwa utaratibu uliopangwa na EWURA na kwa sasa Mafuta ya mwezi wa Juni na Julai tayari yalishaagizwa.
Hata hivyo amesema kuwa changamoto za bei ya mafuta kwa sasa zinachangiwa na mwenendo wa kisiasa Duniani ikiwemo vita ya Urusi na Ukraine hivyo kuathiri uchumi kutokana uhaba wa upatikanaji na uzalishaji wa mafuta.
Kwa upande wao waagizaji na wasambazaji wa mafuta wamesema hakuna uhaba wa Mafuta kuna Mafuta ya kutosha kwenye matenki kwani na meli zinasubiria kushusha mafuta huku nyingine zikiwa njiani kuleta mafuta.
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx