×

Waamuzi Nane Kutoka Afrika Kuchezesha Mechi za Kombe la Dunia Nchini Qatar

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limetangaza orodha ya waamuzi watakaochezesha mechi za michuano ya Kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Novemba 21, mwaka huu na kumalizika Desemba 18 nchini Qatar.

 

Ufaransa ndiye bingwa mtetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Croatia katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Urusi mwaka 2018.

 

Katika orodha hiyo, wapo waamuzi nane (8) kutoka Afrika watakachezesha mechi za Kombe la Dunia mwaka huu.
Waamuzi hao ni Mustapha Ghorbal kutoka Algeria, Redouane Jiyed kutoka Morocco, Bakary Gassama kutoka Gambia na Balmak Tessema kutoka Ethiopia.

 

Wengine ni Victor Gomez kutoka Afrika ya Kusini, Janny Sikazwe kutoka Zambia, Maguette N’diaye kutoka Senegal na Jean-Jacques Ndala kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

KAJALA Kumzalia HARMONIZE, MCHUMBA wa DIAMOND Azua BALAA | HOTPOT…

Leave a Comment