×

Simba Queens Yapiga Hesabu Kali Mzunguko wa Pili, Yapanga Kumaliza Kazi Mapema

Kikosi cha Simba Queens kinachoshika nafasi ya kwanza katika msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara

MENEJA wa Simba Queens inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), Selemani Makanya, amesema baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza wakiwa kileleni, sasa wanaweka mikakati ya kufanya vizuri zaidi mzunguko wa pili.

 

 

Makanya alisema: “Tupo kwenye hatua za mwisho za maandalizi kuelekea mzunguko wa pili, wachezaji wote wapo vizuri na tayari kutetea ubingwa.

 Kikosi cha Simba Queens kikiwa kwenye picha ya pamoja

“Mzunguko wa pili hautokuwa rahisi kwa sababu kila timu itakuja tofauti zaidi ili kuhakikisha zinatimiza malengo yao kwa asilimia kubwa, hivyo lazima tuhakikishe tunafanya kila jitihada kadiri tuwezavyo kwenye mzunguko huu ili tuchukue ubingwa.”

 

Simba Queens inashika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL), ikikusanya Pointi 35 kwenye michezo 11 iliyoshuka dimbani.

 

Leave a Comment