×

Chukwueze Apigilia Msumari wa Mwisho, Aacha Kilio kwa Wajerumani

Samuel Chukwueze raia wa Nigeria akishangilia goli baada ya kuwafunga Bayern Munich na kutinga nusu fainali ya Ligi la Mabingwa Barani Ulaya

VIGOGO Bayern Munich hawataacha kulikumbuka jina la Samuel Chukwueze ambaye alipachika bao lililowafungashia virago katika mchezo wa hatua ya robo fainali.

 

Ni Robert Lewandowski mshambuliaji mahiri wa Bayern Munich alipachika bao la kuongoza dk ya 52 ila liliwekwa usawa zikiwa zimebaki dk 2 mpira kufika ukingoni.

             Villareal imetinga katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya mabingwa barania Ulaya

Villarreal inasonga hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa kuwa robo fainali ya kwanza ilikuwa ni sare ya kufungana bao 1-1.

 

Sasa Kocha Mkuu, Unai Emery wa Villarreal atakutana na Liverpool ama Benfica katika mchezo wa nusu fainali ya Champions League.

Leave a Comment