×

Kampuni ya Uber Yatangaza Kusitisha Huduma Zake Nchini Tanzania, Sababu Zipo Hapa

Uber yasitisha huduma zake nchini Tanzania

KAMPUNI ya Uber imetangaza kusitisha huduma zake nchini Tanzania, huku ikizitaja nauli elekezi za LATRA kama sababu na kudai itarejesha huduma zake nchini pindi kanuni zikibadilishwa.

WALICHOKISEMA KAMPUNI YA UBER KWENYE BARUA YAO YA KUSITISHA HUDUMA

“Tulitegemea kwamba hii ingejumuisha kujenga mazingira wezeshi ili biashara ya ndani na kimataifa inawiri katika njia nzuri na yenye usawa, lakini kwa bahati mbaya, hali ni kinyume na matarajio” imeeleza sehemu ya ujumbe wa Uber kwa wateja wake.

Tumechukua uamuzi mgumu wa kusitisha kwa muda huduma za UberX, UberXL na UberX Saver nchini Tanzania, bidhaa hizi hazitapatikana kuanzia Alhamis ya tarehe 14 Aprili 2022. Kanuni za sasa za usimamizi wa sekta hii zimejenga mazingira ambayo si rafiki na zimekuwa changamoto kubwa katika uendeshaji wa biashara yetu, hadi pale muafaka utakapopatikana, hatutaendelea kutoa huduma za usafiri wa UberX, UberX Saver na UberXL nchini Tanzania.

Tunapenda kuchukua fursa hii kukushukuru kwa dhati – kwa kuchagua mfumo wetu kufanya safari zako jijini Dar es Salaam ambako tumekuwa tukitoa huduma zetu kwa kipindi cha miaka sita iliyopita.

Huu ni wakati mgumu kwetu sote, lakini hii haina maanai kwamba ndio mwisho wa kila kitu. Tuko tayari kushirikiana na mamlaka husika na kuwa na mazungumzo yatakayoleta tija na kujenga mazingira wezeshi na tutarudi na kuendelea na kukupa usafiri wa kutegemewa na wa uhakika ambao umekuwa ukiitumia, baada ya kujiridhisha kwamba mazingira ya kibiashara ni rafiki.

Tunafahamu kwamba hiki ni kipindi kigumu na usumbufu unaotokana na uamuzi huu na tunapenda kukuhimiza uwasiliane nasi kupitia kwenye app ikiwa una maswali yoyote.

Asante Sana, Tanzania!

Timu ya Uber

HARMONIZE AONESHA JEURI YA PESA, AMNUNULIA KAJALA GARI YA BEI MBAYA LENYE JINA LAKE..

Leave a Comment