×

Kajala Kamjibu Harmonize? Atoa Ujumbe Mzito “Heri Kuwa Peke Yako Kuliko Kuwa na Asiyekufaa”

Mwigizaji mkubwa wa Bongo Movies, Kajala Masanja

Harmonize au Konde Boy Mjeshi ni msanii mkubwa nchini Tanzania ambaye umepinduka mwezi mmoja sasa tangu alipoanza harakati za kumuomba x–wake, Kajala Masanja au Mama Pau amrudie.

 

Harmonize au Harmo ambaye ni C.E.O wa Lebo ya Konde Gang amekuwa akifanya mambo kedekede ya kumshawishi Kajala ikiwemo kumnunulia zawadi za kuonesha kwamba alimkosea na anajutia kwa yale aliyomtendea.

 

Harmonize alianza kuonesha ishara za kutaka Kajala amrudie takriban mwezi mmoja uliopita hata kabla ya kutangaza kuachana na Briana Jai; aliyekuwa mpenziwe aliyedaiwa ‘kumukota’ kutoka Marekani.

 

Awali, Konde Boy aweka wazi hali ya kumpenda na kushindwa kumsahau Kajala na ukweli ni kwamba ndiye aliyechangia kuachana kwake na Briana.

“Hatuko pamoja na Briana sababu moja nilimwambia nimetengana na mtu bila kugombana na nampenda sanaa sasa sina uhakika kama nime-move on, lolote linaweza kutokea,” alisema Harmonize.

 

Mwishoni mwa mwezi Machi, 2022, Harmonize aliweka bango lake na Kajala maeneo ya Kinondoni-Manyanya jijini Dar.

 

Harmonize alisema bango hilo lenye maandishi ya Lovers lilimgharimu shilingi milioni 12  za Kitanzania.

 

“Niliweka mimi 100%. Nilitumia milioni 12. Itakuwa pale kwa takriban miezi sita,” alisema Harmonize.

Mapema mwezi Aprili, 2022, Harmonize alikwenda kwenye duka la vito na kununua mkufu wa thamani ambao Kajala alikuwa ameupenda enzi za uhai wa penzi lao.

 

Harmonize alisema alitumia shilingi milioni tano za Kitanzania kupata cheni hiyo.

“Ni tamu sana kutumia pesa zako kwa mtu unayependa. Wakupeleka sasa? 5M kwa dhahabu,” alisema Harmonize.

Hata baada ya hayo yote, Kajala hakusema hata neno moja kuhusu mambo ya Harmonize.

 

Jana Jumapili Aprili 17, 2022, Kajala alitoa ujumbe ambao baadhi ya walimwengu wamedai kwamba alikuwa anamjibu Harmonize.

Kajala anasema kuwa heri mtu kuishi peke yake kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyemfaa.

“Mfano mwema wa heri kuwa peke yako kuliko kuwa na mtu mbaya au asiyekufaa,” anasema Kajala akiambatanisha ya matunda mawili ambapo moja limeharibika na limeanza kuharibu lingine.

Leave a Comment