
POLISI katika Jiji la Los Angeles Marekani wamemtia kizuizini Rapa maarufu ASAP Rocky ambaye ni mpenzi wa mwanadada Rihanna kwa kosa la kumpiga mtu risasi mitaani mwaka 2021.
ASAP Rocky ambaye jina lake halisi ni Rakim Mayers amekamatwa katika uwanja wa ndege wa Los Angeles akiwa kwenye ndege binafsi yeye na mpenzi wake Rihanna wakitokea kisiwa cha Barbados ambako walienda kwa ajili ya mapumziko kufuatia skendo ya rapa huyo kusaliti penzi lao.

Kwa muda mrefu Polisi wamekuwa wakimchunguza ASAP Rocky kutokana na mtu moja kudai uwa alishambuliwa kwa risasi na ASAP Rocky katika mitaa ya Vista Del Mar na Selma Avenues siku ya Novemba 6 kwenye majira ya saa nne na dakika 20 usiku.