×

Msanii wa Nollywood Rita Dominic Aolewa Akiwa na Umri wa Miaka 46

                                                                           Rita Dominic

MASHABIKI wa filamu nchini Nigeria wametumia mitandao ya kijamii kumpongeza msanii wa Nollywood, Rita Dominic, katika siku yake ya harusi.

 

Picha katika mtandao wa Instagram zinamuonyesha bibi harusi Rita Dominic akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni ya Kiigbo kabla ya sherehe hiyo.

 

Baadhi waliandika “Hongera Rita Dominic. Utoto wangu ulikuwa unafuraha nikikuona kwenye televisheni Mungu abariki ndoa yako”

 

“Upendo wa kweli kamwe hauchelewi”

                                               Rita Dominic akiwa na rafiki zake

Dominic, 46, ni mkongwe wa tasnia ya filamu nchini Nigeria na ameigiza katika filamu nyingi maarufu.

 

Harusi hiyo imehudhuriwa na waigizaji wenzake kadhaa wakiwemo Joke Silva, Uche Jombo, Kate Henshaw na Ini Edo.

Leave a Comment