×

Lewis Hamilton na Serena Williams Waungana Kuinunua Klabu ya Chelsea

Dereva wa magari ya Langalanga Lewis Hamilton ameweka kiasi cha paundi milioni 10 kuimiliki Chelsea

BINGWA wa Dunia mara saba katika mashindano ya uendeshaji wa magari ya Langalanga maarufu kama Formula 1 Sir Lewis Hamilton pamoja na Bingwa namba moja katika mchezo wa tenesi kwa wanawake Serena Williams kwa pamoja wameweka kitita cha Paundi milioni 20 ili kuwa wamiliki wapya wa Klabu ya Chelsea.

 

Wanamichezo hao maarufu wameingia ubia kwa kuungana na mwekezaji anayetajwa kuwa na nafasi kubwa ya kuwa mmiliki mpya wa klabu ya Chelsea Sir Martin Broughton.

Serena Williams ameweka kiasi cha paundi milioni 10 kuwa mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea

Muendesha magari ya Langalanga na bingwa wa dunia mara saba katika mchezo huo Sir Lewis Hamilton kwa sasa anaendesha magari ya Kampuni ya Mercedes ambapo kipindi cha nyuma alikuwa aifanya kazi na Kampuni ya Mclaren kuanzia kipindi cha mwaka 2007-2012.

Leave a Comment