
“Makaburi ya pamoja ya wakazi wa Mariupol yanadaiwa kuwa waliouawa na jeshi la Urusi yanafanyika katika kijiji kilicho karibu na baraza la jiji la bandari ya kusini mwa Ukraine linasema.
Katika taarifa yake, inasema wanachimba mitaro ya urefu wa mita 30 (futi 98) na kutumia lori za kutupa taka kuleta miili kwenye eneo lililo nje kidogo ya kijiji cha Manhush, magharibi mwa jiji lililozingirwa.
Halmashauri ya jiji la Mariupol imechapisha picha ya angani zinazodaiwa kuonesha tovuti hiyo, ikisema “tayari ni kubwa mara mbili ya makaburi ya karibu”.

Hata hivyo, kampuni ya teknolojia ya Marekani Maxar inasema kwamba picha zake za hivi karibuni za satelaiti zenye kiwango cha juu “zinaonesha kuwepo kwa eneo la kaburi la watu wengi kwenye ukingo wa kaskazini-magharibi wa Manhush, Ukraine (iko karibu kilomita 20 magharibi mwa Mariupol) na karibu na makaburi ya kijiji kilichopo”.
“Mapitio ya picha zetu za satelaiti kutoka katikati ya Machi hadi katikati ya Aprili yanaonesha kuwa wigo wa seti mpya ya makaburi ulianza kati ya 23-26 Machi, 2022, na umeendelea kuongezeka katika wiki kadhaa zilizopita.
“Makaburi yamepangwa katika sehemu nne za safu za mstari (zinazopima takriban mita 85 kwa kila sehemu) na yana makaburi mapya zaidi ya 200,” Maxar anasema.
Kampuni hiyo ya Marekani pia imechapisha msururu wa picha za satelaiti zinazodaiwa kuonesha eneo la kaburi la watu wengi karibu na Mariupol.