×

Sababu Tatu Kwa Nini Urusi Wanamuogopa Sana Elon Reeve Musk?… Soma Hapa

Elon Reeve Musk

Jina lake halisi ni Elon Reeve Musk, ndiye mtu tajiri kuliko watu wote duniani. Utajiri wake haujaja kupitia kuuza pipi, soda, unga wa ngano n.k kama wengine wanaojiita matajiri, la hasha, yeye umeupata kupitia teknolojia tena ile ya hali ya juu!

 

Hiyo ni sababu ya kwanza inayowapa hofu Urusi. Jamaa ni mwanamapinduzi wa kweli kwenye teknolojia tena ya sayansi ya hali ya juu ambayo pia ndio msingi wa nguvu za kijeshi kwa sasa duniani ambapo vita inafanyika kisayansi sio kwa kupasua matofali kwa vichwa.

 

Sababu ya pili ni kwamba ndiye binadamu wa kwanza wa kujitegemea (siyo serikali) kuishinda Urusi kwenye teknolojia hasa kwenye mambo ya anga na kutawala ulimwengu kwa nyanja za maroketi na satellite zenye teknolojia ya hali ya juu zaidi.

Ikumbukwe kuwa Urusi iliitawala anga kwa kutumia roketi za Soyuz na alipokuja Elon akawachapa na Falcon 9 na Falcon Heavy ambazo ziliweza kwenda na kurudi zikatua kwa ufanisi mkubwa na zikatumika tena tofauti na Soyuz ya Urusi ambayo ikienda, ikirudi inakufa!

 

Sababu ya tatu ni kwamba Warusi wanaamini Elon Musk ndiye binadamu mwenye akili kuliko binadamu wote duniani! Ndiyo, hata mimi naamini hivyo. Ikumbukwe kuwa baba wa sayansi ya roketi ni Mrusi Konstantin Tsiolkovsky na Wamarekani wengi walitumia sayansi yake hiyo hiyo kutengeneza maroketi yao.

 

Mwaka 2015 Elon kupitia kampuni yake ya SpaceX na ujuzi wake binafsi kama mhandisi mkuu akabadili ‘rocket equation’ na kumpa uwezo wa roketi zake kutua bila shida yoyote. Hii ikawaumiza sana vichwa Wamarekani na kumuona kama mtu asiye mtu wa kawaida! Warusi wakapata habari, wakavutiwa nae sana!

Alipojua kuwa wamevutiwa naye akaamua kuandika barua ili awatembelee Warusi. Kremlin kusikia hivyo ikasema Elon mtu wa kuheshimika Urusi nzima hawezi kuandika barua bali wao ndiyo wamwandikie kumuomba awatembelee! Putin kwa mkono wake akacharanga barua, Elon akaipata na akakubali.

 

Kwa bahati mbaya akashindwa kwenda Urusi, Putin akamuomba japo kwa video aongee na wanafunzi wa chuo cha sayansi ya juu cha Urusi, Elon akakubali na kuongea na wanafunzi! Akasimama mwanafunzi mmoja na kuzungumza naye, kwanza akasema: “Leo naongea na kiumbe ambaye si wa sayari hii…” Elon akashtuka kwamba kwa nini huyu bwana mdogo aseme hivi?

 

Sababu ya nneni kwamba mkuu wa mamlaka ya anga za mbali wa Urusi anambembeleza Elon awape ‘equation’ yake mpya ya sayansi ya roketi, anamuomba wakutane na Putin japo waongee, Elon anasema gharama ya kutoa equation yake mpya ni kubwa mno.

 

Ila akakubali kukaa kuzungumza na Putin kwa masuala mengine, Putin akafurahi na kumuomba waziri wake afanye haraka hilo liwezekane, lakini mzozo wa Ukraine ukaingilia kati!

 

Sababu ya tano ni kwamba Elon ndiye mtu anayemiliki mifumo ya mawasiliano mikubwa kuliko hata taifa lolote kupitia satellite za Starlink. Kwa kifupi satellite za starlink zipo zaidi ya 1,500 angani na zinafanya kazi dunia nzima.
Satellite hizi 800, miongoni mwake zipo zile zenye mifumo ya ku-detect makombora. Pia Starlink ni bora zaidi ukilinganisha na Cosmos za Urusi.

 

Sababu ya sita ni kwamba yeye mshirika mkuu wa Jeshi la Anga la Marekani huku akipewa kushika jeshi maalum la anga za mbali (U.S Space Force) likiwa na kituo chake angani ambako wamekiwekea mitambo ya kutogunduliwa na teknolojia yoyote isipokuwa ya kwao tu.

 

NDOTO ZA ELON MUSK
Katika mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni aliwahi kusema kuwa ili ndoto zake zitimie ni lazima ahamie nchini Marekani, hivyo alifanya kila namna ahame nchini Afrika Kusini kwenda Marekani japo wazazi wake hawakupenda.

 

1. NDOTO YAKE YA KUTOA HUDUMA YA INTERNET BURE DUNIA NZIMA
Mpaka Sasa kampuni yake ya safari za anga SpaceX imefanikiwa kufunga satellite zaidi ya 60 duniani kote na alipohojiwa alikiri kuwa na ndoto za kutoa huduma za data bure miaka ya usoni

 

2. NDOTO YA KUHIFADHI KUMBUKUMBU ZA WATU KIELEKTRONIKI
Pia bilionea huyu mtaalam wa programu za kompyuta, alizindua mpango wake wa kuhifadhi kumbukumbu za binadamu kwa njia ya data kwa kutengeneza mfumo wa chip ambazo zitakuwa zikifanya kompyuta iwasiliane na ubongo na kuchukua taarifa

 

3. KUITAWALA SAYARI YA MARS
Pia kampuni ya spaceX imefanikiwa sana katika safari za kwenda sayari ya Mars na kufanya tafiti za mbali, mwenyewe akitumia kauli mbiu ya ‘aim to colonize Mars’ akimaanisha ‘lengo la kuitawala sayari ya Mars’.
Huyo ndiyo Elon Musk, mwamba anayeogopwa sana na Urusi!
Imeandaliwa na Emanuel Msoka, unaweza kuwasiliana naye kwa namba 0769421630.

Leave a Comment