
Kwa mujibu wa shirika la habari la Interfax la Urusi, jeshi la Urusi limefanikiwa kupata udhibiti kamili wa eneo lote la mkoa wa Kherson, pamoja na sehemu za miji ya Kharkiv, Zaporizhzhia na Mykolaiv.
Katika hotuba yake kwa taifa Jumanne usiku, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alikiri Warusi walikuwa wakijaribu kuweka nguvu ya udhibiti katika eneo lililotekwa.
“Waliendelea kushambulia askari wetu karibu na Kharkiv, huko Donbas,” alisema. “Wanajaribu kuonyesha madai ya ‘serikali mpya’ huko Kherson na sehemu ya eneo la Zaporizhzhia.”

Kituo cha utawala cha kikanda cha Kherson, jiji la Kherson, kilitekwa katika siku za mwanzo za vita. Lakini Pentagon baadaye ilisema wanajeshi wa Urusi walikuwa wamepoteza udhibiti wake. Kherson ndio eneo lenye idadi kubwa zaidi ya watu inayoshikiliwa na Urusi hadi sasa.
Rais Putin alidai Jumanne kwamba mapigano huko Mariupol yamemalizika. Mji huo wa kimkakati wa bandari ya kusini umekumbwa na mashambulizi ya Urusi ambayo yaliwaacha wapiganaji wapatao 1,000 wa Ukraine wakiwa wamezingirwa.