AFISA Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli leo Aprili 27, 2022 akiwa kwenye kipindi cha Krosi Dongo cha @255globalradio amesema msimu huu watani zao wa jadi Simba hawatapata taji lolote kwani vinara hao wa ligi kuu wanataka kuchukua mataji yote.
Ameongeza kuwa kwa sasa Simba taji pekee wanalowaza ni kuifunga Yanga, timu hizo zitacheza Jumamosi Aprili 30 mchezo wa ligi kuu bara.