×

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango Atoa Heshima za Mwisho Akiaga Mwili wa Mwai Kibaki

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tatu wa Kenya,  Mwai Kibaki. Ibada ya kuaga mwili huo imefanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi nchini Kenya.

Rais Uhuru Kenyatta ameongoza maelfu ya Wakenya katika maombolezo ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Nchi hiyo, Mwai Kibaki leo Aprili 29, 2022 katika Uwanja wa Nyayo

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria ni Makamu wa Rais wa Tanzania; Dkt. Philip Mpango, Rais Salva Kiir (Sudan Kusini), Rais Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini) na Sahle Work-Zewde (Ethiopia)

Kibaki alikuwa Rais wa Kenya kuanzia 2002 – 2013, na alifariki dunia akiwa na miaka 90.

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Leave a Comment