×

Ujasusi wa Marekani Unaisaidia Ukraine Kuwauwa Maafisa wa Ngazi ya Juu wa Urusi – NY Times

Rais Joe Biden.

Marekani imevipatia vikosi vya Ukraine ujasusi ambao umewasaidia kuwalenga na kuwauwa majenerali wa Urusi katika Ukraine, kulingana na ripoti kutoka gazeti la New York Times, likiwanukuu maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani.

Maelezo ya shuguli za vikosi vya Urusi na mahala vilipo vikosi vyake vinavyo hama hama vinaaminiwa kuhusisha ujasusi wa marekani , na ulitumiwa na vikosi vya Ukraine wakati wa mashambulio ambayo yalipelekea kuuawa kwa maafisa wa kijeshi wa Urusi.

Maafisa wa Ukraine wanadai Majenerali 12 wa ngazi ya juu waliuawa katika mzozo, huku ikidhaniwa kuwa morali ya chini miongoni mwa wanajeshi wa Urusi imewalazimisha maafisa wa ngazi ya juu jeshini kwenda karibu zaidi na maeneo ya mapigano.

Hawakubainisha ni mangapi kati ya mashambulio haya walisaidiwa na ujasusi wa Marekani.

Msemaji wa Ikulu ya White House alikosoa taarifa ya gazeti la New York Times, akisema kichwa chake cha habari kilikuwa “kinapotosha” na “kutowajibika”.

Msemaji wa Baraza la usalama la taifa, Adrienne Watson aliongeza kuwa Marekani huipatia Ukraine ujasusi unaohusu uwanja wa mapambano ili ‘’kulinda nchi yao’’ na bila “lengo la kuwauwa Majenerali Warusi.”

SIMBA WAMEKUBALI Ubingwa WAMEUKOSA, MASTAA YANGA Waapa KUBEBA UBINGWA | SPORTS ZONE..

Leave a Comment