
KOREA KASKAZINI imefyatua kombora jingine kutoka kwenye nyambizi ya kivita ambalo limesafiri na kutua nje kidogo ya eneo la kiuchumi la nchi ya Japan.
Korea Kaskazini imefanya hivyo ikiwa zimebaki siku mbili tu kabla ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol ambaye amesema atapambana na Pyongyang.
Taarifa kutoka Korea Kusini zinadai Korea Kaskazini ilifyatua ombora la masafa marefu kutoka kwenye Nyambizi ya Kivita muda wa saa 5:07 kutoka pwani ya mashariki katika miji ya Sinpro, ambako Pyongyang ina yadi kubwa ya Meli.
Wizara ya Ulinzi ya nchi ya Japan imebainisha kuwa kombora hilo linaweza kuwa la masafa marefu, Shirika la Utangazaji la Umma la Japana NHK likinukuu taarifa iliyotolewa na Serikali ya nchi hiyo limethibitisha kuwa kombora hilo limetua nje kidogo ya mji wa kiuchumi wa nchi hiyo.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameagiza Maafisa wote kujiandaa na hali isiyodhanika ikiwemo makombora kutoka Korea Kaskazini na kuhakikisha usalama wa Ndege pamoja na Meli, japokuwa hakukuwa na taarifa yoyote ya madhara yaliyojitokeza kutokana na mlipuko huo.
Kufyatuliwa kwa kombora hilo limekuwa ni jaribio la kwanza kwa nchi ya Korea Kaskazini kufyatua kombora la masafa marefu kutoka kwenye nyambizi ya kivita kwa kipindi kirefu tangu ifanye hivyo mwezi Oktoba mwaka jana ambapo ilifyatua kombora la masafa mafupi kutoka 8.24 Yongung.
Kombora hilo limekuwa la 15 ndani ya mwaka huu tu, ikiwemo jaribio la hivi karibuni la kombora la masafa marefu la bara moja hadi jingine ambalo mara ya mwisho kujaribiwa kabla ya hivi sasa ilikuwa ni mwaka 2017.
Robert Kelly, Mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Pusan kilichopo nchini Korea Kaskazini amedai kufyatuliwa kwa kombora hilo ni salamu kwa mtawala mpya wa Korea Kusini ambaye anaingia madarakani hivi karibuni kumuonesha msimamo na uwezo wa kivita wa Korea Kaskazini.

Kelly amenukuliwa akiliambia Shirika la Habari la Aljazeera akisema:
“Nafikiri wazo ni kutuma ujumbe kwa watu wa Korea Kusini, bado tupo inabidi mtuwekee umakini mkubwa, Korea Kaskazini wana utamaduni na mazoea ya kufanya hivi ikiwa ni mjumuiko wa kutuma ujumbe lakini pia vitisho kwa nchi nyingine.”
Mwezi uliopita Rais wa Korea KaskazinI Kim Jong Un alisema serikali yake inadhamiria kuendelea kutengeneza makombora na zana nyingine za kivita kwa spidi ya hali ya juu kwa kuthibitisha hilo Kim Jong Un hivi karibuni ameonekana akikagua gwaride la maonesho ya silaha ambalo lilionesha silaha za makombora ya masafa marefu ya kutoka bara moja hadi jingine na makombora ya masafa marefu kutoka kwenye Nyambizi za Kivita.