
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza kuzishikilia paspoti za wafanyakazi wa Kampuni ya Gas Entec Shipbuilding Engineering inayojenga Meli mpya ya Mv.Mwanza Hapa Kazi tu katika Bandari ya Mwanza Kusini ambayo itagharimu zaidi ya shilingi billion 97 ambapo mpaka sasa Serikali imelipa zaidi ya asilimia 80 ya fedha zote.

Majaliwa amesema lengo la kuchukua uamuzi unatokana na Kampuni hiyo kuondoa wafanyakazi zaidi ya 100 waliokuwa wanajenga Meli hiyo na kubakiza wafanyakazi 20 jambo lingine ni Kampuni hiyo kuuza hisa kwa Kampuni nyingine bila Serikali kujua jambo ambalo ni kinyume na mkataba wa Kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania.