
FINLAND imesema haiogopi vitisho vya Urusi na kudai kwamba kuungana kwao na Muungano wa Kijeshi wa NATO utaleta thamani kubwa, Waziri anayeshughulikia Masuala ya Ulaya, Tytti Tuppurainen amesema wakati wa mahojiano na Sky News.
Msukumo wa Finland kutaka uanachama wa NATO, umechochewa na mzozo wa Ukraine na Tuppurainen anasema:
“kwa manufaa ya Finland na uhuru wa uendeshaji wa harakati za kitaifa, ndiyo umeongeza msukumo zaidi.”

Anakubali kwamba, inajulikana kwa miaka mingi kwamba Kremlin haipendelei upanuzi wa NATO, lakini alisisitiza kwamba hatua hiyo haikusudii kuchochea makabiliano na Moscow (Urusi).
“Tuko tayari kwa kila aina ya nia mbaya na hatua mbaya dhidi yetu. Lakini hakuna hofu kabisa. Hatuogopi,” Tuppurainen amesema.
Cc; @sifaelpaul