×

Kombora la Majeshi ya Urusi Lateketeza Kituo cha Kijeshi Nchini Ukraine

Moshi mzito ukitokea eneo ngome ya kijeshi ya Ukraine lililoshambuliwa na kombora la Urusi

KITUO cha kijeshi cha Lviv nchini Ukraine kimeharibiwa vibaya na shambulio la kombora la Urusi, Gavana wa eneo hilo, Maksym Kozytskyy amesema kwenye Telegram.

 

Katika wiki za hivi karibuni, Urusi imekuwa ikilenga mashambulizi yake Mashariki mwa Ukraine, lakini mashambulizi ya hapa na pale yameendelea katika maeneo ya Magharibi kama vile Lviv.

 

“Makombora manne ya adui yalipiga kituo cha miundombinu cha kijeshi katika Mkoa wa Lviv.

Eneo la ngome ya kijeshi lililoshambuliwa likifanyiwa marekebisho

“Kituo hicho kimeharibiwa kikamilifu, Kulingana na taarifa za awali hakukuwa na majeruhi,” Kozytskyy amesema.

 

Ameongeza kuwa, mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine imedungua makombora mawili.

 

Mapema jana, Kozytskyy alisema makombora hayo yalipiga kituo hicho saa 04:30 kwa saa za huko.

Cc; @sifaelpaul

Leave a Comment