×

Kocha wa Mbeya Kwanza Afungiwa Miaka Mitano, Namungo Wapewa Pointi 3

Kocha wa Mbeya Kwanza, Mbwana Makata na Meneja David Naftali wamefungiwa kwa kipindi cha miaka mitano (5) kila mmoja kwa kosa la kushawishi/kuamuru wachezaji wasiingie uwanjani kuanza mchezo kati ya Namungo dhidi ya Dodoma Jiji, tukio lililosababisha mchezo usifanyike na kuchafua taswira ya Ligi ikiwemo kusababisha hasara kwa wadhamini wa Ligi.


Mechi ya hiyo haikufanyika kwasababu Mbeya Kwanza iligoma kucheza kwa kile walichoeleza kuwa ni kutokamilika kwa moja ya taratibu za maandalizi ya mchezo (uwepo wa gari la kubebea wangonjwa kwenye uwanja wa Ilulu, Lindi kabla ya kuanza mchezo huo).

Wachezaji wa timu ya Namungo wakifanya mazoezi.

Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipa Namungo FC pointi 3 na magoli matatu ambazo amepokwa Mbeya Kwanza kwa kugomea kucheza mechi katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi baada ya gari ya kubebea wagonjwa kuchelewa kufika na wao wakisema kikanuni ni dakika 15 zinatakiwa kusubiri na TPLB imesema kwa mujibu wa kanuni ni dakika 30.

Leave a Comment