Rais Samia Azindua Barabara ya Nyahua – Chaya, Tabora Yenye Urefu wa KM 85.4 (Picha +Video)
Global Publishers May 17, 2022 0 Comments
SHARE THIS:
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya Sita inaendelea kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoanza wakati wa serikali ya awamu tano huku akisisitiza kuwa miradi mingi imeanza kukamilika.
Rais Samia amesema hayo Mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa barabara ya Nyahua – Chaya Mkoani Tabora yenye urefu wa KM 85.4 ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanza katika serikali ya awamu ya tano ambapo amesema wanaosema serikali yake imeiacha baadhi ya miradi ni uongo
Rais Samia akiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED) Waleed SH. Albahar, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila, akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Barabara ya Nyahua-Chaya yenye 85.4 km katika Sherehe zilizofanyika Tura, Uyui mkoani Tabora tarehe 17 Mei,2022.
Aidha Rais Samia amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu inayojengwa na serikali ikiwemo barabara na madaraja ili iweze kudumu na kuchangia katika maendeleo
Rais Samia pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED) Waleed SH. Albahar wakitoa kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Nyahua-Chaya 85.4 km kwenye Sherehe za ufunguzi wa barabara hiyo katika Kijiji cha Tura, Uyui mkoani Tabora tarehe 17 Mei, 2022. Wengine katika picha ni Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani.
Katika hatua nyingine Rais Samia amewaagiza mawaziri kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za UVIKO – 19 zinazotumika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo huku akisema mwisho wa matumizi ya fedha hizo ni mwezi ujao (June) mwaka huu, ambapo amemuagiza Waziri wa Tamisemi kuhakikisha anasimamia tenda zote kukamilika kwa wakati
Rais Samia akizungumza na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED) Waleed SH. Albahar mara baada ya Sherehe za ufunguzi wa barabara ya Nyahua-Chaya.Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait (KFED) Waleed S. Albahar wakati akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando ya barabara ya Nyahua-Chaya mara baada ya ufunguzi.Viongozi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akiwahutubia katika Sherehe za ufunguzi wa barabara ya Nyahua-Chaya 85.4 km zilizofanyika katika Kijiji cha Tura, Uyui mkoani Tabora tarehe 17 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akifungua barabara ya Nyahua – Chanya (km 85.4) katika kijiji cha Tura, Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora leo tarehe 17 Mei, 2022.