×

Maua: Walinizushia Nimefariki ili Wanipoteze Kwenye Tasnia ya Muziki

Msanii wa zamani wa muziki wa asili Maua Chenkula

MSANII mkongwe wa nyimbo za asili Maua Chenkula amefanya mahojiano ndani ya studio za 255globalradio na Global TV ambapo amethibitisha kuwa zile taarifa zilizosambaa kipindi cha nyumba kwamba Maua alifariki zilikuwa ni za uongo zenye lengo la kumpoteza kwenye ramani ya muziki.

 

“Nafikiri walifanya vitu vyoote wakaona haijatosha, wakaona kwamba huyu tukimtangazia kifo watu si watajua amekufa! Kwahiyo walinitengenezea hilo tukio ili wanipoteze kwenye muziki” alisema Maua.

 

Pamoja na mahojiano ya kina Maua aligoma kabisa kuweka wazi kuwa ni nani aliyetaka kumuua au kupanga njama za kupoteza kwenye ramani ya muziki.

Maua Chenkula anadai alizushiwa kifo ili kumpoteza kwenye ramani ya muziki

Katika mahojiano yake amebainisha kuwa moja ya misukosuko na changamoto kubwa aliyokutana nayo katika safari yake ya muziki ni kuchomwa kisu akiwa anajiandaa na tamasha la muziki mkoani Mara ambapo alichomwa kisu kwenye shingo na mtu asiyejulikana lengo likiwa ni kupoteza uhai wake.

 

Mbali na hayo Maua amegusia pia ushindani wake kimuziki na mwanamuziki mwenzie kutoka mkoani Kagera Saida Karoli, amedai kwamba yeye ndiye alikuwa msanii wa kwanza kuibuka kwa kuanza kuimba nyimbo za asili kabla hata ya umaarufu wa Saida Karoli lakini alifanyiwa hujuma baada ya Saida Karoli kupewa Promo kuliko yeye na hivyo kufanya Saida kuonekana kama mwanzilishi wa kuimba nyimbo za asili.

 

Maua Chenkula alitamba na nyimbo ya akatambala iliyomtambulisha kwenye ramani ya muziki nchini lakini pia nje ya nchi.

 

 

 

 

Leave a Comment