×

Ajali Imetokea Morogoro Baada ya Gari Kugonga Behewa la Treni

Eneo la tukio ambapo gari limegonga behewa la Treni

AJALI mbaya imetokea inayohusisha gari aina ya TOYOTA PICKUP lenye namba ya usajili T 840 DQF lililokuwa likitokea maeneo ya Tumbaku kuelekea Msamvu kugonga Behewa la Treni lililokuwa likitokea Kilosa kuelekea Stesheni ya Morogoro.

Behewa la Treni likiwa limekandamiza gari aina ya Toyota Pick Up

Tayari Askari wa Usalama Barabarani wameshafika eneo la tukio na shughuli za uokoaji zimeendelea sambamba na uchunguzi wa tukio hilo.

Leave a Comment