×

Rais Samia Ashiriki Mdahalo wa Wakuu wa Nchi Accra, Ghana Ataja Changamoto Tatu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika Mdahalo pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nchi nyingine kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB kujadili fursa mbalimbali pamoja na changamoto zinazolikabili Bara la Afrika. Mkutano huo wa 57 wa AfDB unafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.

 

Rais Samia Suluhu Hassan akishiriki Mdahalo wa Wakuu wa Nchi uliofanyika Accra, Ghana ametaja changamoto tatu ambazo amekutana nazo tangu awe Rais wa Tanzania

Amesema “Changamoto kubwa ya kwanza ilikuwa kuaminiwa. Mwanamke wa kwanza kushika nafasi kubwa, kuwafanya watu wa Tanzania waniamini, nilifanikiwa hilo”

Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.


Anaongeza “Niliongoza Nchi vizuri kama Wanaume wanavyofanya, inawezekana zaidi ya kile walichokuwa wamefanya wao. Pili, ilikuwa kukabiliana na UVIKO-19 na tatu ni kuyumba kwa uchumi kutokana lakini tulipamba, kwa ushirikiano wa washirika na mambo yakaanza kwenda vizuri”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa amesimama na Rais wa Ghana Mhe. Nana Akufo-Addo, Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina pamoja viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 57 wa AfDB unaofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Accra nchini Ghana tarehe 24 Mei, 2022.

Leave a Comment