
MANCHESTER United italazimika kutoa pauni 115m kwa wachezaji wawili ambao wanapewa kipaumbele katika usajili ujao.
Wachezaji hao ni beki wa Ajax, Jurrein Timber na straika wa Benfica, Darwin Nunez ambao wametisha katika msimu uliomalizika hivi karibuni.
Inaelezwa kuwa, katika fedha hizo ambazo United itatoa, pauni 35m kwa ajili ya Timber na pauni 80m za Nunez.
Ripoti zinaeleza kuwa, Kocha Erik ten Hag ameupa kipaombele zaidi usajili kwani anaamini utakuwa msaada ndani ya kikosi chake.
Ten Hag alifanya kazi na Timber ndani ya Ajax kwa muda wote beki huyo alicheza mechi 74, akafunga mabao manne na asisti mbili tangu mwaka 2020.
Man United inapambana kujenga kikosi chake upya baada ya msimu wa 2021/22 kufanya vibaya.
Wakati United ikitoa pauni 80m kwa Nunez, asilimia 20 ya fedha ya usajili itaenda kwa klabu yake ya zamani ya Almeria.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa kocha huyo mpya anaweza kuleta sura mpya sita ndani ya Man United. Ingawa hii itatagemeana na wale wachezaji ambao wataondoka kikosini hapo.
MANCHESTER, England