×

Chawa Pro Max, Baba Levo Kufanya Sajari ya Pua na Kitambi Nchini Uturuki

Baba Levo alifanikiwa kupata mualiko wa kuhudhuria ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa pamoja na Boss wake Diamond Platnumz

 

CHAWA Pro Max, yeye hupenda kujiita Fundi Manyumba ‘Baba Levo’ amesema ana mpango wa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa pua na kitambi kwani amekuwa akichekwa mara nyingi kutokana na muonekano wake huo.

 

Baba Levo amesema; ”Nakwenda Uturuki kuhakikisha nafanya surgery ya pua maana nimechekwa vya kutosha.

Baba Levo amesema atafanya upasuaji wa kurekebisha pua yake

“Sasa ni muda umefika niende kufanya surgery, niende nikate pua niwe handsome boy, itagharimu kama shilingi milioni 46 za Kitanzania kwa sababu ni pua na kitambi,” amesema Baba Levo.

Leave a Comment