×

LeBron James Aweka Rekodi ya Kuwa Bilionea wa Kwanza Anayecheza Kikapu

LeBron James amekuwa Bilionea wa kwanza mcheza kikapu ambaye bado anaendelea na mchezo huo

MCHEZAJI wa Kikapu kutoka Timu ya Los Angeles Lakers na mshindi mara nne wa Ligi ya NBA LeBron James ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kikapu wa kwanza kuwa Bilionea kwa wachezaji ambao bado wanacheza ukimtoa Michael Jordan ambaye alikuwa Bilionea baada ya kustaafu mchezo huo.

 

Kwa mujibu wa jarida la Forbes Supastaa huyo wa Timu ya Los Angeles Lakers ametengeneza zaidi ya dola bilioni 1.2 kupitia kukua kwa biashara zake lakini pia mishahara yake anayopata katika Ligi ya NBA kwa muda wa miaka 19 ambayo imemkusanyia zaidi ya dola milioni 383 na ametengeneza zaidi ya dola milioni 900 kupitia mikataba ya matangazo ya biashara.

 

James alikuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuwa Bilionea kwani mwaka 2014 alipohojiwa na GQ alinukuliwa akisema:

 

“Ni adhima yangu kubwa, kiukweli nataka kukuza biashara zangu. Na kama itatokea nikapata, kama nikiwa Bilionea mwanamichezo, mungu wangu! Ntajisikia faraja sana.”

James akiwa katika majukumu yake na timu yake ya Los Angeles Lakers

Uwekezaji mwingine mkubwa kwa LeBron James ni kwenye Televisheni na Studio ya kutengeneza muvi ya SpringHill Entertainment ambapo anatengeneza zaidi ya dola milioni 300 kwa mujibu wa takwimu za Jarida la Forbes, Studio hiyo ilisaidia kutengeneza Space Jam: A New Legacy Muvi ambayo yeye mwenyewe alishiriki na ikamuingizia kiasi cha dola milioni 163.

Leave a Comment